Bible & Mission Centre ilianzishwa mwaka 2017 katika mji wa Arusha. Kanisa letu limejikita katika kufundisha Neno la Mungu, kufanya kazi za umisheni, na kuhudumia jamii. Tumekuwa na ushirikiano mzuri na maeneo jirani na tumejenga jamii ya waamini wenye imani thabiti.
Tunaamini katika Mungu mmoja aliye katika nafsi tatu. Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Bwana wetu Yesu Kristo kuwa ni Mungu aliyedhihirishwa katika mwili, kwa kuzaliwa na bikira, maisha yake ya kibinadamu yasiyo na dhambi, miujiza yake ya kiungu, kifo chake cha upatanisho, ufufuo wake wa kimwili, kupaa kwake, na kurudi kwake binafsi katika uwezo na utukufu
Tunaamini katika maandiko matakatifu ambayo kimsingi yametolewa na Mungu, yamevuviwa na Mungu, hayakosei, yanaaminika kabisa, na ni mamlaka kuu katika masuala yote ya imani na mwenendo. Wokovu wa wanadamu walipotea na wenye dhambi; damu ya Yesu krito iliyomwagika, kwa imani wala si kwa matendo na kuzaliwa upya na Roho Mtakatifu husafisha dhambi.
Roho Mtakatifu ambaye hukaa ndani ya mwamini humuwezesha kuishi maisha matakatifu, kushuhudia, na kufanya kazi kwaajili ya Bwana Yesu Kristo. Ufufuo wa wafu (yaani waaminio) kwa hukumu na uzima wa milele au adhabu katika jehanamu
Tunaamini pia katika umoja hivyo tunafanya kazi kwa ushirikiano na makanisa yote ya kiinjili, huduma zote, mashirika ya makanisa na jamii kwa ujumla.
Kuwafanya waamini wote kuwa wanafunzi wa Yesu na kufanana na sura ya kristo. Kufanya kazi ya kuwainua waamini waliojitoa na ambao wataibadilisha jamii yao katika kila nyanja ya maisha, na kuhubiri neno la Mungu, sifa na kuabudu, pamoja na maombi
Kuwawezesha washirika kumwelekea Mungu, kisha wao kwa wao katika uhusiano wa kweli, Kuwatia moyo, pamoja na kuwafikia wale ambao bado hawajaunganishwa na familia ya Mungu. Kwa kuzingatia kanuni za kibiblia, kanisa litawaandaa watu katika ujuzi mbalimbali wa maisha na maarifa ya kiroho.
Bible Mission Centre, Arusha, Tanzania
Tunaamini na kufundisha Biblia kuwa ni Neno la Mungu.
Maombi ni msingi wa kanisa letu.
Tunaongozwa na upendo wa dhati kwetu sisi wenyewe, majirani, marafiki, na jamii tunayoitumikia.
Tunafanya kwa ubora wa hali ya juu katika kila kazi na katika utendaji wetu wote.